Kiswahili

Tarehe 17 mwezi wa 10, 2011 shughuli ya kijamii katika eneo la Kisanga
Mwaka huu tunasheherekea siku ya kutokomeza umaskini uliokithiri si tu kwa kupitia kusanyiko hili dogo la watu kwa shuhuda, mashairi, ngonjera, n.k. Pia tunaadhimisha kwa vitendo kwa kuungana na jamii katika shughuli ya kijamii ambayo kati yenu tayari mmeshashiriki jana na leo…Jarida la Aprili 2012
Kwenye warsha ya ATD Dunia ya Nne mwezi Aprili, "Tufanye kazi pamoja kama washirika walio sawa", tutawaleta pamoja watu wanaoishi kwenye umaskini uliokithiri na watu wenye nyadhifa katika nyanja mbalimbali ili kushirikishana mawazo na uzoefu wao. Warsha itashereheshwa na maneno ya mwanzilishi wa ATD Dunia ya Nne, Joseph Wresinski, na raisi wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, ambao wana mawazo yenye mvuto na yanayofanana kuhusu umaskini…Jarida la Februari 2012
Wiki chache zilizopita, ilikuwa mwanzo wa mwaka mpya wa shule, muda wa kufurahia kwa watoto wengi, furaha za kuwa wanafunzi au kukutana na wanafunzi wenzao tena. Hata hivyo, kwa baadhi ya watoto, mwanzo wa mwaka wa shule ni wakati mgumu : kushindwa kuandikishwa kwa darasa la kwanza, umbali wa shule za secondary, kupata matatizo kwenye malipo yanayoagizwa shuleni…Jarida la Disemba 2011
Salehe, mwanachama wa kikosi cha wanaharakati wa kujitolea ameombwa kujiunga na timu ya Marekani (USA). Baada ya ushuhuda wake tutaelezea maana ya kikosi cha wanaharakati wa kujitolea."Machozi ya mtu maskini Tanzania ni sawa na machozi ya mtu maskini Uingereza au Marekani..."








